Uandaaji wa Mihutasari na Vitabu vya Elimu ya Dini ya Kiislamu kidato cha I-IV

Mwaka 1996, IPC ilishiriki katika warsha ya uundaji wa mihutasari mipya ya “Elimu ya Dini ya Kiislamu” kidato cha I - IV na “Islamic Knowledge” kwa kidato cha V - VI na Diploma ya Ualimu iliyofanywa na jopo la dharura la “Islamic Education Panel”.

Pia Machi,1996, IPC ilishiriki katika warsha ya wiki tatu ya kuandika vitabu vya kiada vya Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa kidato cha I - IV Baada ya jopo lile la muda kumalizika kazi yake ya kuandika miswada ya vitabu hivyo vinne, IPC ilikabidhiwa jukumu la kuvihariri na kuvichapisha.

Pia jukumu la kuandaa miswada ya vitabu vya kiada vya ‘A’ level na Diploma iliachiwa IPC na kazi ile ya jopo la dharura ikaishia pale. Kwa uwezo wa Allah (s.w), kufikia Oktoba, 1998 kitabu cha kwanza cha Elimu ya Dini ya Kiislamu Shule za Sekondari kilitoka na kufikia 2001 vitabu vyote vinne (4) vilichapishwa na kuwa mashuleni na mitaani chini ya usimamizi wa IPC.

NEXT/ENDELEA